book cover

MPAKA LINI?

By: chuchu

Lindsey ni mama wa watoto wanne anayejaribu kuishi maisha ya ukamilifu na furaha huku akijitahidi kuokoa ndoa yake inayoelekea kuangamia. Jitihada zake zinagonga mwamba pale anapogundua kuwa mume wake ana mahusiano ya muda mrefu na mwanamke ambaye sasa ni mjamzito. Hilo linampelekea Lindsey kukata tamaa na kuanza kufuatilia talaka. Lakini mume wake Adrian hayuko tayari kumuachia, kuna watoto ambao Lindsey anatamni wakue na baba yao. Lakini Maisha ya Lindsey yanazidi kuvurugika anapokuja kuangukia kwenye penzi la kijana mdogo daktari. Kuna sababu nyingi za wao kutokuwa pamoja lakini upendo ulioko baina yao unawavuta pamoja. Je upendo pekee utatosha kuvuka changamoto zote? Ungana nami katika safari hii ya maisha ya Lindsey naamini utaburudika na kuelimika. By Chuchu


Namba ya Simu